• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  MAN UNITED YAICHAPA WAKATI WOLVES 1-0 MOLINEUX


  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Molineux Stadium mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Marcus Rashford dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya Bruno Fernandes.
  Na kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya nne, ikiizidi pointi mbili Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi 16.
  Kwa upande wao Wolves baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 13 za mechi 17 sasa nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA WAKATI WOLVES 1-0 MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top