• HABARI MPYA

  Tuesday, December 27, 2022

  TAFSIRI ZA KISHERIA NA SABABU ZA FEISAL KUVUNJA MKATABA YANGA...

  Na Oscar Oscar, Dar es Salaam
  TATIZO kubwa la nchi yetu, kila anayejua Lugha ya Kiingereza anadhani anaweza Kutafsiri Document ya Kisheria. 
  My dear brothers and sisters, Sheria ina Tafsiri tofauti kabisa na Kiingereza tunachoombea Maji ya kunywa! Feisal anaweza kuvunja Mkataba wake na Yanga wakati wowote lakini ni lazima kuwe na extraordinary circumstances (i.e kacheza chini ya 10% ya mechi zote za Yanga, kama hajalipwa Mshahara kwa miezi miwili mfululizo, kama kuna makubaliano yoyote na Klabu ambayo hayajatekelezwa yenye uwezo wa kuathiri performance yake uwanjani). Ili kifungu alichotumia Feisal kuvunja Mkataba kiwe halali ni lazima mambo hayo hapo juu yote au Moja liwe halijatekelezwa. Kuna chochote Yanga hawajampa? Jibu ni hapana. Kapewa kila kitu.

  Kinachotusumbua watanzania wengi ni Mentality za Ki-Socialism na Uswahili! Aziz KI akilipwa 20M, na wewe unataka kupewa hiyo hiyo. Bernard Morrison akipewa Gari, na wewe unataka upewe wakati si sehemu ya makubaliano kwenye mkataba wako na Muajiri! Mara nyingi unapotokea Mgogoro wa Mchezaji na Klabu, Majority husimama upande wa mchezaji na kuhisi anaonewa! Hawa wachezaji wanalijua hilo na sasa wanaanza ku-take advantage. Mshahara wa Feisal wa 4M haukuwa unajulikana lakini umevujishwa juzi Makusudi ili Jamii imuonee Huruma!
  The reason behind was to gain public Sympathy! My dear brothers and sisters, Feisal hakulazimishwa kusaini Mkataba wa mshahara wa 4M kwa mwezi. Feisal hakuwa amevuta Mpepe wakati wa kusaini. Alisaini akiwa na Akili timamu. 4M miaka miwili iliyopita ilikuwa inamfanya kuwa miongoni mwa Wazawa wanaolipwa vizuri tu nchini.
  Tunawapenda wachezaji wetu lakini tuwasaidie kupita njia zilizonyooka. Mambo ya kupita sana kwa Mpalange hayawasaidii. Feisal alipaswa kufungua njia ya kuwa mchezaji mzawa aliyeuzwa na kukunuliwa kwa Bei Ghali zaidi nchini. Wanaomtaka Feisal, wasipite Uchochoroni kwa Mpalange. Waende wakazungumze na Yanga wamalizane.
  Kimsingi hakuna mahali ambapo Yanga wamemkosea Feisal. Hakuna. Walioko nyuma ya Mchezaji ni watu hatari sana. Sitaki kuamini kama 112M alizolipa Feisal zinatoka mfukoni mwake. Siamini. Hawa watu waliomshawishi Feisal wakiachiwa, kesho watafanya the same kwa Clatous Chama.
  (Oscar Oscar ni Mwandishi wa Habari na mtangazaji wa kituo cha Redio na Televisheni cha EFM)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAFSIRI ZA KISHERIA NA SABABU ZA FEISAL KUVUNJA MKATABA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top