• HABARI MPYA

  Saturday, December 03, 2022

  DODOMA JIJI YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 LITI


  TIMU ya Dodoma imeendelea kujiinua kutoka eneo la hatari baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Dodoma Jiji leo yamefungwa na Salum Kipaga aliyejifunga dakika ya nne na Hassan Mwaterema dakika ya 24, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Ally Bilal dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC wanakamilisha mechi zao 15 za mzunguko wa kwanza wakiwa na pointi 15 na kusogea nafasi ya 12, wakati Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao 11 za mechi 15 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top