• HABARI MPYA

  Saturday, December 03, 2022

  SIMBA SC YAIBUTUA COASTAL UNION 3-0 MKWAKWANI


  TIMU ya Simba SC imekamilisha mzunguko was kwanza was Ligi Kuu kwa ushindi was mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja was Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Wazambia, mshambuliaji Moses Phiri mawili dakika ya 56 na la pili kwa penalti dakika ya 61, wakati la tatu limefungwa na kiungo Clatous Chama dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 34 katika mchezo wa 15 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Coastal Union baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 12 za mechi 14 nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIBUTUA COASTAL UNION 3-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top