• HABARI MPYA

  Friday, December 02, 2022

  SINGIDA BIG STARS YAICHAPA NAMUNGO FC 3-0 LITI

  WENYEJI, Singida Big Stars wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na kiungo mzawa, Said Hamisi Ndemla dakika ya 28 na washambuliaji Mnyarwana, Meddie Kagere dakika ya 65 na Mrundi, Amissi Tambwe dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Namungo inabaki na pointi zake 18 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAICHAPA NAMUNGO FC 3-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top