• HABARI MPYA

  Thursday, December 02, 2021

  UCHAGUZI WA BODI YA LIGI KESHO MORO


  UCHAGUZI wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) sasa utafanyika kesho katika hoteli ya Cate mjini Morogoro.
  Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili  Kiomoni Kibamba leo imesema kwamba uchaguzi utatanguliwa na Mkutano wa Baraza Kuu la TPLB Saa 3:00 asubuhi.
  Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndiye mgombea pekee aliyepitishwa kuwania tena nafasi hiyo baada ya kuenguliwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Mbette Msolla na wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI WA BODI YA LIGI KESHO MORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top