• HABARI MPYA

    Friday, October 20, 2017

    WATATU YANGA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA OKOBA 28

    Na Adam Hhando, TABORA
    YANGA itaondoka mchana wa leo mjini Tabora kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Stand United Jumapili, lakini kocha Mzambia, George Lwandamina anafahamu wachezaji wake watatu tegemeo wako hatarini kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu Oktoba 28.
    Mabeki Juma Abdul na Kelvin Yondan pamoja na kiungo Raphael Daudi wote walionyeshwa kadi za njano za pili Jumamosi Uwanja wa Kaitaba, Yanga ikishinda 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
    Kwa sababu hiyo, watatu hao hawahitaji nyongeza ya kadi kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Oktoba 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Kiungo Raphael Daudi amesajiliwa msimu huu kutoka Mbeya City

    Kuna uwezekano mkubwa, kocha Lwandamina akawapumzisha wachezaji hao kwenye mechi ya Jumapili kuhofia wasionyeshwe kadi zaidi wakaukosa mchezo muhimu dhidi ya mahasimu.
    Lakini pia kutokana na tatizo la beki ya kati katika kikosi cha Yanga msimu huu, haitakuwa ajabu Yondan akachezeshwa Jumapili ingawa kwa beki ya kulia hakuna shaka Hassan Kessy anaweza kucheza badala ya Abdul. 
    Katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers uliofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Lwandamina aliwaanzisha pamoja katika beki ya kati Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
    Cannavaro amekuwa hatumiki sana msimu huu na ni kama anajiandaaa kustaafu baada ya kuitumikia klabu tangu mwaka 2006 – lakini hainaamishi hawezi kuhimili tena vishindo vya Ligi Kuu.
    Beki mwingine wa kati Yanga ni Abdallah Hajji ‘Ninja’ ambaye aliingia dakika ya 65 na akaenda kumalizia vizuri mechi dhidi ya Rhino timu hizo zikitoa sare ya 0-0, wakati kuna Pato Ngonyani pia ambao wote wanaweza kumudu mechi zisizo na presha kubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATATU YANGA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA OKOBA 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top