• HABARI MPYA

  Thursday, October 05, 2017

  SINGIDA UNITED WAANZA KUITAMBIA YANGA MAPEMAAA

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  SINGIDA United imeanza kuitishia nyau Yanga baada ya kusema kuwa, mabingwa hao watetezi waanza kujiandaa kisaikolojia kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi yao, mchezo uatakaopigwa Novemba 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Namfua Singida.
  Akizungumza na Mtandao wa Bin Zubeiry Sports – Online, Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, alisema kuwa, Yanga wanahitaji kuajiandaa kisaikolojia kabla ya mchezo huo kwani watakuwa wametoka kwenye mechi ngumu dhidi ya Simba na wanakwenda kukutana nao.
  Alisema, mechi hiyo ya kwanza kwao katika Uwanja huo ambao haujatumika tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu kutokana na kuwa katika ukarabati, wanajiandaa kuonyesha soka safi mbele ya mabingwa hao watetezi lakini pia kwa mashabiki wa timu hiyo mkoani humo.
  Singida kwa sasa wanatumia Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani ambapo kwa sasa wapo katika maandalizi yake kuelekea mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting, Oktoba 14 mwaka huu.
  Timu hiyo inatarajiwa kuwafuata Ruvu, Oktoba 12 mwaka huu kwenda Pwani kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mabatini Pwani.
  “Timu ipo katika hali nzuri, tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Ruvu, lakini baada ya hapo tutakwenda kucheza na Ndanda kabla ya kuwavaa Mtibwa Sugar ambapo kote wanahitaji kukusanya jumla ya pointi tisa kwenye mechi hizo zote.
  “Baada ya mechi hizo, tunarudi kwenye Uwanja wetu wa nyumbani wa Namfua, Singida kucheza na Yanga, mchezo utakuwa na ushindani wa hali ya juu kwani tunahitaji kuonyesha soka la hali ya juu hivyo wapinzani wetu wajiandae kisaikolojia,” alisema Sanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAANZA KUITAMBIA YANGA MAPEMAAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top