MSHAMBULIAJI wa Colombia, Radamel Falcao ameingia lawamani akituhumiwa kuwaambia wachezaji wa timu pinzani wacheze pole pole ili watoe nao sare katika mechi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi.
Radamel Falcao (kushoto) anadaiwa kuwarubuni wachezaji wa Peru wasiifunge Colombia mechi ya kufuzu Komne la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Colombia na Peru walitoka sare ya 1-1 mjini Lima, wageni wakitangulia kwa bao la James Rodriguez ambaye alipewa pasi na Falcao mwenyewe.Falcao na timu yake ya taifa walimenyana na jirani zao wa Amerika Kusini, Peru Jumanne jioni, mchezo ambao ilishuhudiwa Colombia wakikata tiketi ya kwenda Urusi mwakani.
Radamel Falcao (kushoto) anadaiwa kuwarubuni wachezaji wa Peru wasiifunge Colombia mechi ya kufuzu Komne la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Link hii pic.twitter.com/8laXomElvY inaonyesha namna ambavyo Falcao alikuwa anawashawishi wachezaji wa Peru mmoja baada ya mwingine kucheza watoe sare.
Peru ilisawazisha kupitia shujaa wa taifa lake, Pablo Guerrero dakika ya 76.
Baada ya kupata bao lao, wachezaji wa Peru wakaendelea kucheza kwa nguvu kabla ya Falcao kuwafuata kuwaambia wapunguze makali mechi iishe kwa sare.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea alionekana kuwasogelea wachezaji wa Peru mmoja mmoja kuwapa ujumbe huku akionekana kumsukuma mchezaji mwingine akampe ujumbe na mwenzake.
Na tangu hapo mchezo ukapooza kutokana na dhamira ya kucheza uishe kwa sare kama ulivyomalizika kwa timu hizo kufungana 1-1.
Na kwa matokeo hayo, Colombia imefuzu moja kwa moja Kombe la Dunia wakati Peru watakwenda kwenye mchujo wa kuwania kwenda Urusi mwakani na watamenyana na New Zealand nyumbani na ugenini mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment