• HABARI MPYA

  Friday, October 06, 2017

  BAYERN MUNICH YATHIBITISHA KUMREJESHA JUPP HEYNCKES

  Bayern Munich imetangaza kumrejesha kocha wake wa zamani, Jupp Heynckes kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  REKODI YA HEYNCKES BAYERN MUNICH 

  1987-91: P198, W113, D46, L39 W% 57.1
  2009: P 5, W 4, D1 L0 W% 80
  2011-13: P109 W83 D12 L14 W% 76.2
  JUMLA: P312 W200 D59 L53 W% 64.1
  MATAJI: Bundesliga x3 (1989, 1990, 2013), German Cup (2013), Champions League (2013)
  KLABU ya Bayern Munich imetangaza kumrejesha kocha wake wa zamani, Jupp Heynckes, ambaye ataiongoza timu kwa muda hadi mwishoni mwa msimu kufuatia kuondoka kwa Carlo Ancelotti.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 72 hajafundisha klabu tangu alipoondoka Bayern Munich akiiachia mataji matatu msimu wa 2012-13, lakini analazimika kurejea kazini akitoka kustaafu.
  Heynckes amesema: "Nisingerudi kwenye klabu nyingine yoyote duniani, lakini Bayern Munich ni kazi ya mapenzi kwangu. Makocha wangu wasaidizi na mimi sasa nitafanya kila kitu kurejesha mafanikio kwa mashabiki wa soka. Ninaangali mbele sana juu ya changamoto hii,".'
  Mtendaji Mkuu, Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Kuna imani kubwa baina ya Jupp Heynckes na Bayern. Tunamshukuru sana Jupp kwamba amekubakli ofa ya kuwa kocha mkuu. Ni mtu bora kwa wakati huu Bayern,".'
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH YATHIBITISHA KUMREJESHA JUPP HEYNCKES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top