• HABARI MPYA

    Friday, December 09, 2016

    KIPA MGHANA AFANYA VITU SI MCHEZO SIMBA YAWAPIGA POLISI

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    KIPA mpya Mghana wa Simba SC, Daniel Agyei ameonyesha kiwango kikubwa leo timu hiyo ikiifunga 2-0 Polisi Moro ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Kipa huyo aliyesajiliwa mapema wiki hii kwa mkataba wa miaka miwili kutoka klabu ya Medeama ya Ghana, alidaka kwa dakika zote 90 leo mabao ya Simba yakifungwa na kiungo Abdi Banda na mshambuliaji Ibrahim Hajib.
    Kipa mpya wa Simba, Mghana Daniel Agyei ameanza vizuri leo akiiongoza timu kushinda 2-0 dhidi ya Polisi Moro Uwanja wa Jamhuri 

    Kiungo mpya aliyeletwa kwa majaribio kutoka Ghana pia, James Kotei alipewa muda mfupi wa kucheza akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Muzamil Yassin na hiyo ni kwa sababu alifika kambini jana tu, hivyo hakuwa na mazoezi ya kutosha.
    Kikosi cha Simba kilikuwa;Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Abdi Banda, Novat Lufunga, Method Mwanjali, Muzamil Yassin/James Kotei, Shiza Kichuya/Hija Ugando, Said Ndemla/Jonas Mkude, Laudit Mavugo/Ibrahim Hajib, Frederick Blagon/Mohammed Ibrahim na Jamal Mnyate/Mussa Ndusha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA MGHANA AFANYA VITU SI MCHEZO SIMBA YAWAPIGA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top