• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 24, 2016

  AC MILAN WABEBA SUPER CUP YA ITALIA, WAIDUNDA JUVE KWA MATUTA DOHA

  Wachezaji wa AC Milan wakisherehekea na taji lao la Super Cup ya Italia baada ya kuwafunga wapinzani wao wakubwa wa Serie A, Juventus kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Jassim Bin Hamad (Al-Sadd) mjini Doha, Qatar jana. Giorgio Chiellini alianza kuifungia Juventus dakika ya 18 akimalizia kona ya Miralem Pjanic, kabla ya Giacomo Bonaventura kuisawazishia AC Milan dakika 20 baadaye akimalizia krosi ya Suso.
  Gianluca Lapadula na Mario Mandzukic walikosa penalti zao kabla ya kipa wa Milan Gianluigi Donnarumma kuokoa vizuri na kuipa timu yake Super Cup ya saba katika historia yao PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AC MILAN WABEBA SUPER CUP YA ITALIA, WAIDUNDA JUVE KWA MATUTA DOHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top