• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 22, 2016

  MWANASOKA BORA AFRIKA NI AUBAMEYANG, MANE AU MAHREZ

  KIUNGO wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang atachuana na mawinga Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mane wa Senegal kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2016 baada ya watatu hao kuingia fainali ya kinyang'anyiro cha tuzo hiyo.
  Watatu hao wameingia fainali baada ya kura zilizopigwa na Makocha wakuu au Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama na Mashirikisho ya Soka ya nchi wanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Kamati ya Vyombo vya Habari, Kamati ya Ufundi na Soka na jopo la wataalamu wa vyombo vya Habari. 
  Hiyo inamaanisha Mohamed Salah wa Misri na Islam Slimani wa Algeria wameishia kwenye tanp bora.
  Katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, kipa wa Uganda, Dennis Onyango ameingia fainali na mshambuliaji wa Zimbabwe, Khama Billiat na kiungo wa Zambia, Rainford Kalaba.
  Washindi watatajwa katika sherehe za usiku wa tuzo za CAF Alhamisi ya Januari 5 mwaka 2017 mjini Abuja, Nigeria.
  Ikumbukwe Aubameyang anatetea tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, wakati tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika imeachwa wazi na mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe, Mbwana Samatta aliyehamia KRC Genk ya Ubelgiji Januari mwaka huu kufuatia kushinda tuzo hiyo, taji la Ligi ya Mabingwa na kuwa mfungaji bora akiwa na klabu ya DRC. 

  Pierre-Emerick Aubameyang atachuana na Riyad Mahrez na Sadio Mane kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2016 

  ORODHA KAMILI YA TATU BORA;
  Mwanasoka Bora wa Afrika
  Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund)
  Riyad Mahrez (Algeria na Leicester City)
  Sadio Mané (Senegal na Liverpool)
  Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika
  Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns)
  Khama Billiat (Zimbabwe na Mamelodi Sundowns)
  Rainford Kalaba (Zambia na TP Mazembe)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWANASOKA BORA AFRIKA NI AUBAMEYANG, MANE AU MAHREZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top