• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 23, 2016

  KIONGOZI WA ZAMANI WA 'MABAUNSA' AFARIKI DUNIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanyanyua Tanzania (TWLA), Mpoki Bukuku amefariki dunia leo.
  Bukuku, aliyekuwa mpiga picha wa kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa magazeti la Nipashe, The Guardian na Lete raha, amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
  Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.
  "Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Mwenge  (ITV), taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas.
  Mpoki Bukuku (kushoto) akiwa na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete
  Bukuku (kushoto) akiwa na Mwandishi nguli wa habari za michezo nchini, Masoud Saanan

  Mpoki Bukuku amewahi pia kufanya kazi kampuni za Business Times Limited (BTL) na Mwananchi Communication Limited (MCL) kabla ya kujiunga na Guardian. Marehemu ameacha mke na watoto. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIONGOZI WA ZAMANI WA 'MABAUNSA' AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top