• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 24, 2016

  HAJIB AENDA HARAS EL HODOUD YA MISRI KWA MAJARIBIO

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib ameondoka nchini jana kwenda Misri kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya huko.
  Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba, Hajib amekwenda huko kwa baraka zote za uongozi kufuatia klabu hiyo kutuma barua ya mwaliko.
  “Tofauti na inavyosemwa kwamba Hajib ametoroka, ni kwamba huyu kijana amekwenda Misri kwa Baraka zote za uongozi na atakuwa huko kwa wiki moja akifanya majaribio,”amesema Kaburu.
  Ibrahim Hajib (kulia) ameondoka jana kwenda Misri kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa

  Amesema kabla ya kumruhusu, uongozi uliwasiliana na benchi la Ufundi kuomba maoni yao juu ya hilo na ukatoa baraka zake aende, ukiamini hataacha pengo katika timu.
  Kaburu amesema kwamba si sera ya Simba kuwazuia wachezaji wanapopata nafasi nje, ndiyo maana na Hajib ameruhusiwa, hivyo amewataka wachezaji wote wanapopata nafasi waombe ruhusa badala ya kufikiria kutoroka.
  Hajib aliondoka jana siku moja kabla ya timu yake kumenyanana JKT Ruvu leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam walioshinda 1-0. 
  Na mshambuliaji huyo ameonyesha kiu ya kweli ya kutaka kucheza nje ya Tanzania, kwani katikati ya mwaka huu alikwenda Afrika Kusini kwa majaribio pia, ambako pamoja na kuripotiwa kufuzu katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJIB AENDA HARAS EL HODOUD YA MISRI KWA MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top