• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 30, 2016

  YANGA KUMKOSA BOSSOU KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itaondoka jioni ya kesho kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kesho visiwani humo.
  Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam tayari kwa safari ya leo majira ya Alasiri.
  Yanga itaondoka na kikosi wachezaji 26 pamoja na benchi lake zima la ufundi tayari kwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya pemba Saa 2.30 usiku wa kesho.
  Vincent Bossou hatakuwepo kwenye kikosi cha Yanga Kombe la Mapinduzi kwa sababu anakwenda AFCON

  Kikosi kamili cha Yanga kinachokwenda Zanzibar ni makipa; Deogratius Munishi 'Dida', Benno Kakolanya na Ali Mustafa 'Barthez'.
  Mabeki ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Pato Ngonyani, Vincent Andrew, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Juma Abdul na Oscar Joshua.
  Viungo ni Haruna Niyonzima, Justin Zulu, Simoni Msuva, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashuiya, Deus Kaseke, Saidi Juma 'Makapu', Thabani Kamusoko na Yussuf Mhilu.
  Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe, Emmanuel Martin, Obrey Chirwa na Matheo Anthony. 
  Katika michuano hiyo, Yanga SC itamkosa beki wake Mtogo, Vincent Bossou aliyekwenda nchini Senegal kujiunga na timu yake ya taifa, Togo kwa maandalizi ya mwisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Januari 14, 2017 nchini Gabon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA KUMKOSA BOSSOU KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top