• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 22, 2016

  PALACE YAMTUPIA VIRAGO PARDEW, ALLARDYCE KUCHUKUA NAFASI

  KLABU ya Crystal Palace imemfukuza kocha wake, Alan Pardew na itakutana na wawakilishi wa Sam Allardyce baadaye leo.
  Palace inataka kocha huyo wa zamani wa England achukue nafasi ya Pardew haraka iwezekanavyo ili aiongoze timu katika Ligi Kuu ya England. 
  Pardew anafukuzwa Uwanja wa Selhurst Park baada ya kiasi cha miaka miwili ya kufanya kazi na klabu hiyo. Na anaiacha katika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, juu ya nafasi za hatari za kushuka daraja. 
  Mwenyekiti wa Palace, Steve Parish amesmhukuru Pardew kwa mchango wake  katika klabu hiyo ikiwemo kuwapa Kombe la FA msimu wa 2015-16.
  Crystal Palace imemfukuza kocha Alan Pardew baada ya matokeo mabaya msimu huu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PALACE YAMTUPIA VIRAGO PARDEW, ALLARDYCE KUCHUKUA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top