• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 21, 2016

  FANJA ‘WAIFANYIA MTIMANYONGO’ MBEYA CITY ITC YA NGASSA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  FANJA FC ya Oman ‘inawafanyia mtimanyongo’ Mbeya City kwa kutotuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa ya mchezaji Mrisho Ngassa.
  Ngassa ameachana vizuri na Fanja mapema mwezi huu baada ya kuwa nayo kwa miezi miwili na kuwafungia bao moja katika mechi mbili za Ligi na kurejea nyumbani kujiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Lakini uongozu wa Mbeya City umelalamika kwamba tangu wiki iliyopita umekuwa ukifanya jitihada kubwa za kupata ITC ya Ngassa bila mafanikio. 
  Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Mbeya City akitokea Fanja ya Oman


  “Tunafanya juhudi kubwa tu, tunawapigia simu jamaa (Fanja) tunazungumza nao vizuri, wanasema wanauma, lakini hawatumi, basi tu,”alisema Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana usiku.
  Baada ya kukosa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar wakilazimishwa sare ya 0-0 nyumbani, Mbeya City wanapambana ITC ya Ngassa ipatikane ili acheze mechi ijayo dhidi ya Toto Africans Jumamosi Uwanja wa Sokoine, Mbeya pia.
  Ngassa alitua Fanja akitokea Free State Stars ya Afrika Kusini alikosajiliwa na kocha wa sasa wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri.
  Kisoka, Ngassa aliibukia Toto Africans ya Mwanza, kabla ya kwenda Kagera Sugar, Yanga SC, Azam FC, Simba na baadaye Jangwani tena.
  Wakati huo huo: Beki Haruna Shamte yuko hatarini kuukosa mchezo dhidi ya timu yake ya zamani, Toto Africans baada ya kuumia kwenye mchezo na Kagera.
  Ofisa habari wa MCC, Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea  mchezo huo  yanaendelea  vizuri na wachezaji wote wakiwa na ari kubwa, ingawa Shamte hajafanya mazoezi baada ya kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FANJA ‘WAIFANYIA MTIMANYONGO’ MBEYA CITY ITC YA NGASSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top