• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 31, 2016

  MBEYA CITY YAIPIGA 3-1 MBAO FC SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  MBEYA City imezinduka na kuifumua Mbao FC mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya huku mshambuliaji Zahor Pazi aking’ara zaidi.
  Pazi, mchezaji wa zamani wa Azam FC, Simba na JKT Ruvu amefunga bao moja, huku linguine likikataliwa na refa.
  Mabao mengine ya MCC inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri yamefungwa na Rapahel Alpha na Tito Okelo, wakati la Mbao FC lilifungwa na Kwenye mchezo huo Mbao ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia Rajesh Kotecha.
  Ushindi huo unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 18 na kupanda hadi nafasi ya sita.
  Mchezo mwingine leo, Mwadui imeshinda mechi ya tatu mfululizo chini ya kocha mpya, Ally Bushiri baada ya kuilaza 2-1 Kagera Sugar Uwanja wa Mwadui Complex, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
  Mshambuliaji Zahor Pazi amefuga bao moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbao FC leo 

  Ushindi huo, unaifanya Mwadui FC sasa kufikisha pointi 22 baada ya mechi 18 na kujivuta juu kwa nafasi nne kutoka ya 13 kwenye ligi ya timu 16. 
  Katika mchezo huo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la Themi Felix Buhaja, kabla ya Awadh Juma kusawazisha na Razack Khalfan kufunga la pili kipindi cha pili.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAIPIGA 3-1 MBAO FC SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top