• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 21, 2016

  LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA

  KIUNGO mshambuliaji wa Liberty Professionals, Latif Blessing amechaguliwa Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Ghana msimu wa 2015/2016. 
  Winga huyo machachari ambaye alikuwa ana msimu mzuri na klabu hiyo ya Accra, amewapiku viungo Kwasi Donsu wa Medeama na Abdul Bashiru wa Dream FC kushinda tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika Ijumaa iliyopita mjini Accra. 
  Blessing pia alishinda tuzo ya mfungaji bora wa msimu wa Ligi Kuu y Ghana kwa mabao yake 17 aliyofunga. 
  Mchezaji wa Hearts of Oak, Inusah Musah ameshinda tuzo ya beki bora wakati mlinda mlango Richard Ofori wa mabingwa wa Ligi,  Wa All Stars amekuwa kipa bora.
  Mchezaji Bora na mfungaji bora wa Ligi ya Ghana, Latif Blessing wa Liberty Professionals (kushoto) akipokea tuzo yake

  WASHINDI WOTE WA TUZO
  Mchezaji Bora wa Msimu -   Latif Blessing (Liberty Professionals)
  Mfalme wa Mabao - Latif Blessing (Liberty Professionals)
  Kipa Bora wa Msimu - Richard Ofori (Wa All Stars)
  Beki Bora wa Msimu  - Inusah Musah (Hearts of Oak)
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu - Abdul Alidu Hudu
  Klabu Bora ya Msimu - Wa All Stars (kwa kushinda taji la ligi)
  Kocha Bora wa Msimu - Anos Adipa (Wa All Stars)
  Mtendaji Mkuu Bora wa Msimu - Oduro Nyarko (Wa All Stars)
  Tuzo ya mchezo wa kiungwana- Berekum Chelsea
  Refa Bora wa Msimu - Awal Mohammed
  Mpiga picha Bora wa Msimu - Paul Agbeyagah
  Kamisaa Bora wa Msimu -  Augustine Asante
  Mshika Kibendera Bor wa Msimu -  Haruna Bawa
  Tuzo ya heshim- Welbeck Abra-Appiah (Mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya Ligi)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top