• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 26, 2016

  MTIBWA SUGAR WAENDA KUISUBIRI KWA HAMU MAJI MAJI MANUNGU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Salum Mayanga wa Mtibwa Sugar amesema kwamba anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Maji Maji ya Songea Desemba 28, mwaka huu.
  Baada ya ushindi wa mabao 2-0 juzi dhidi ya wenyeji Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, mabao ya viungo Haroun Chanongo na Vincent Barnabas, Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani Uwanja wa Manungu Desemba 28 kuikaribisha Maji Maji.
  Salum Mayanga (kulia)amesema kwamba anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao dhidi ya Maji Maji 

  Na Mayanga ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online kwamba baada ya ushindi wa Jumamosi, anaelekeza nguvu kwenye mchezo ujao dhidi ya Maji Maji kwa lengo la kwenda kuendeleza wimbi la ushindi.
  Mayanga alisema kwamba wanaiheshimu Maji Maji ambayo kwenye mchezo uliopita walitoa sare ya 0-0 na Azam FC mjini Songea na kwamba hawataidharau hata kidogo.
  Kutokana na ushindi huo wa juzi, Mtibwa Sugar sasa inafikisha pointi 27 sawa na Azam FC baada ya timu zotre hizo kucheza mechi 17 na zinafungana nafasi ya nne na ya tano, zikizidiwa pointi moja na Kagera Sugar katika nafasi ya tatu.
  Simba SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 41 baada ya kucheza mechi 17, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 37 za mechi 17 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAENDA KUISUBIRI KWA HAMU MAJI MAJI MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top