• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 21, 2016

  YANGA WAPEWA WABABE WA COMORO, WAKIVUKA WANA ZANACO AU APR...AZAM WARUKA KIHUNZI

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za awali za michuano ya klabu Afrika mwakani, Kombe la Shirikisho Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa na wababe wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Ngaya de Mbe ya Comoro.
  Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam FC wao wataanzia Raundi ya kwanza ambako watamenyana na mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.
  Yanga wataanzia ugenini wikiendi ya Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano wikendi ya Februari 17 hadi 19, mwaka huu.

  Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

  Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza. Na Yanga wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

  RATIBA KAMILI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
  RATIBA KAMILI KOMBE LA SHIRIKISHO 2017
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA WAPEWA WABABE WA COMORO, WAKIVUKA WANA ZANACO AU APR...AZAM WARUKA KIHUNZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top