• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 25, 2016

  PHIRI ASEMA MBEYA CITY ILIKOSA BAHATI TU JANA NBELE YA TOTO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mmalawi wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwamba walikosa bahati tu ili kushinda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tananua dhidi ya Toto Africans ya Mwanza juzi.
  Mbeya City ililazimishwa sare ya pili mfululizo juzi nyumbani, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya baada ya kutoa 0-0 na Toto Africans ya Mwanza ikitoka kutoa sare ya 0-0 na Kagera Sugar ya Bukoba wiki iliyotangulia.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, kocha huyo wa zamani wa Free State Stars ya Afrika Kusini amesema kwamba vijana wake walijituma na kupeleka mashambulizi langoni mwa Lyon, lakini wakashindwa kufunga.
  Wachezaji wa Toto Africans wakipita kuwasalimia wachezaji wa Mbeya City jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya

  “Sisi tumeshambulia sana na tulitarajia angalau tungepata hata bao moja, lakini wapinzani wetu walicheza kwa kujihami zaidi, maarufu kama kupaki basi. Tunasema kwa leo (jana) wamefankiwa, ila sisi tunasonga mbele kwenye maandalizi ya mchezo ujao,”alisema. 
  Pamoja na hayo, Phiri amemsifu kipa wa Toto, Mussa Kirungi kwa kuokoa michomo mingi ya hatari na kuikatalia kabisa Mbeya City kupata bao.
  Baada ya mchezo huo wa juzi, City itacheza mechi ya tatu mfululizo nyumbani itakapoikaribisha Mbao FC Uwanja wa Sokoine Desemba 31, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PHIRI ASEMA MBEYA CITY ILIKOSA BAHATI TU JANA NBELE YA TOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top