• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 31, 2016

  NGASSA AREJEA LIGI KUU LEO MBEYA CITY IKICHEZA NA MBAO SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa anarejea kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo baada ya msimu mmoja.
  Ngassa alihamia Free State Stars ya Afrika Kusini kutoka Yanga ambako alicheza kwa msimu mmoja, kisha kwenda Fanja ya Oman alikodumu kwa miezi miwili na kurejea Tanzania kujiunga na Mbeya City.
  Wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili kwenye viwanja tofauti, Ngassa naye anatarajiwa kucheza tena baada ya kukosekana kwa muda mrefu.
  Mrisho Ngassa anarejea leo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya msimu mmoja

  Ngassa, kiungo wa zamani wa Azam, Simba na Yanga alishindwa kucheza mechi mbili za awali za Mbeya kutokana na kuchelewa kwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
  Aidha, Mbeya City pia inatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mshambuliaji wake mpya, Zahor Pazi ambaye pia alikwama kucheza kutokana na kuchelewa kwa ITC yake. 
  Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wenyeji Mwadui wataikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba, wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wenyeji Mbeya City watawakaribisha Mbao FC.
  Mchezo kati ya Mwadui na Kagera unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua ukikutanisha timu jirani mikoa za ya Kanda ya Ziwa zinazoundwa na wachezaji wanaofahamiana vizuri.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Toto Africans wataikaribisha Stand United na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, African Lyon wataikaribisha JKT Ruvu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AREJEA LIGI KUU LEO MBEYA CITY IKICHEZA NA MBAO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top