• HABARI MPYA

    Wednesday, December 21, 2016

    ZLATAN AMSAFISHIA NJIA NDUGU YAKE ATUE MAN UNITED

    MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic anaamini Msweden mwenzake, Victor Lindelof ana kipaji kung'ara katika timu kubwa duniani kufuatia kukua kwa tetesi za beki huyo wa Benfica kujiunga na Manchester United Januari.
    United imeingia kwenye mazungumzo na Rais wa Benfica, Luis Felipe Vieira juu ya uhamisho wa Pauni Milioni 38 Januari kwa ajili ya beki huyo wsa kati, ambaye amecheza mechi 11 za kimataifa.
    Na Ibrahimovic, ambaye alifikisha mabao 16 msimu huu baada ya kufunga mabao mawili mswishoni mwa wiki katika ushindi dhidi ya West Brom, amempigia debe mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
    "Yeye (Lindelof) anakuwa. Ana majukumu mengi ya timu ya taifa sasa,"alisema Ibrahimovic. "Ni mzuri kiasi cha kutosha kwa United? Nafikiri yuko tayari kwa klabu kubwa nje ya huko. Ni juu yake anataka nini na mazingira yanasemaje. Chochote atakachochagua, itakuwa vizuri kwake.
    Manchester United wapo kwenye mazungumzo na Benfica juu ya uhamisho wa Pauni Milioni 38 wa beki Victor Lindelof PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZLATAN AMSAFISHIA NJIA NDUGU YAKE ATUE MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top