• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 27, 2016

  SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK YAGONGA MTU 2-0

  Na Mwandishi Wetu, DAE ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi leo na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
  Genk ilikuwa inacheza kwa mara ya kwanza leo bila ya kocha wake Mbelgiji Peter Maes iliyemfukuza jana na ikafanikiwa kushinda.
  Samatta aliingia dakika ya 51 kwenda kuchukuaa nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelisn wakati huo tayari Genk inaongoza 2-0 mabao ya Pozuelo dakika ya 19 na Karelis kwa penalti dakika ya 26.
  Maes ndiye aliyemsajili Samatta Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na akamuamini haraka na kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
  Leo Samatta amecheza mechi ya 36 Genk,18 msimu uliopita na 18 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Ndidi, Heynen, Pozuelo/Susic dk89, Bailey/Trossard dk81, Buffalo and Karelis/Samatta dk51.AA Gent : Rinne, Neto, Mitrovic Saief/Verstraete dk66, Nielsen/Desmet dk66, Perbet, Simon Foket, Esiti. Dejaegere) Gershon and Milicevic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK YAGONGA MTU 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top