• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 23, 2016

  LWANDAMINA AWAANZISHA PAMOJA NA NIYONZIMA NA TAMBWE LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina leo amewaanzisha kiungo Haruna Niyonzima pamoja na mshambuliaji Amissi Tambwe katika safu ya ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya African Lyon.
  Yanga wanamenyana na African Lyon jioni ya leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Lwandamina amefanya mabadiliko kidogo katika safu yake ya ushambuliaji.
  Tofauti na ilivyozoeleka Mrundi, Amissi Tambwe hucheza Mzimbabwe Donaldo Ngoma, lakini leo amemmpanga na Mnyarwanda Niyonzima.
  Kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Saidi Juma, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke.
  Katika benchi watakuwapo Ali Mustafa 'Barthez', Hassan Kessy, Andrew Vincent 'Dante', Justin Zullu, Obrey Chirwa, Emmanuel Martin na Geofrey Mwashiuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWAANZISHA PAMOJA NA NIYONZIMA NA TAMBWE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top