• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 30, 2016

  YANGA KUVUNA PONTI ZA CHEE LEO KAMATI YA SAA 72

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA inaweza kukomboa pointi mbili ilizopoteza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya African Lyon baada ya sare ya 1-1 Desemba 23, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba Kamati ya Saa 72 ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kukutana leo kujadili taarifa mbalimbali na kupitia rufaa – huku Yanga wakijiweka mkao wa kuvuna pointi za mezani.
  Hiyo inafuatia rufaa yao waliyomkatia mchezaji wa Lyon, Venence Joseph Ludovic aliyefunga bao la Lyon katika sare hiyo ambaye inadaiwa ni mchezaji halali wa Mbao FC ya Mwanza.
  Venence Ludovic alichezea Mbao FC mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu

  African Lyon inadaiwa kukiuka taratibu za kumsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Mwanza na rufaa mbili zimegongana mezani Bodi, moja ya Yanga na nyingine ya Mbao.
  Zote, Mbao na Yanga zinapinga Ludivic kuichezea Lyon akiwa mchezaji halali ya Mwanza ambayo aliichezea mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa na Mbao, inaonekana kabisa Ludovic alihamia Mbao kimakosa na akatumika kimakosa pia, hivyo Yanga inaweza kushinda rufaa hiyo na kuvuna pointi mbili zaidi.
  Kamati pia leo itapitia Rufaa ya Ndanda FC dhidi ya wachezaji wa Simba kutoka Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei ambao wanadaiwa kucheza mechi baina ya timu hizo wakiwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini.  
  Kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 18, nyuma ya Simba SC yenye pointi 44 za mechi 18 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA KUVUNA PONTI ZA CHEE LEO KAMATI YA SAA 72 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top