• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 31, 2016

  MWADUI YAIPIGA 2-1 KAGERA SUGAR

  Na Mwandishi Wetu, MWADUI
  MWADUI imeshinda mechi ya tatu mfululizo chini ya kocha mpya, baada ya kuilaza 2-1 Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mwadui Complex, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
  Ushindi huo, unaifanya Mwadui FC sasa kufikisha pointi 22 baada ya mechi 18 na kujivuta juu kwa nafasi nne kutoka ya 13 kwenye ligi ya timu 16. 
  Katika mchezo huo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la Themi Felix Buhaja, kabla ya Awadh Juma kusawazisha na Razack Khalfan kufunga la pili kipindi cha pili.  
  Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo Mwadui wanashinda baada ya kuwa chini ya kocha Ally Bushiri, ikitoka kuwafunga Toto Africans na Mbao FC wote 1-0 Uwanja wa Mwadui Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWADUI YAIPIGA 2-1 KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top