• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 26, 2016

  BENIK AFOBE AITWA DRC KIKOSI CHA AWALI AFCON 2017

  KOCHA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Florent Ibenge ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 31 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwakani.
  Mtu muhimu anayekosekana ni winga wa Everton, Yannick Bolasie ambaye anasumbuliwa na maumivu ya goti ambayo yatamfanya azikose fainali hizo.
  Nyota wa Bournemouth, Benik Afobe ambaye ameamua kuchezea The Leopards baada ya kuchezea kikosi cha vijana cha England chini ya umri wa miaka 21, amepewa nafasi na Ibenge.

  Benik Afobe ameitwa kwenye kikosi cha The Leopards kwa ajili ya AFCON ya Januari mwakani 

  DRC imepangwa Kundi C pamoja na Morocco, Ivory Coast na Togo.
  Kikosi kamili cha awali cha DRC kinaundwa na makipa: Nicaise Mulopo Kudimbana (Royal Antwerp, Ubelgiji), Ley Matampi (TP Mazembe), Joel Kiassumbua (FC Wohlen, Uswisi).
  Mabeki: Chancel Mbemba (Newcastle, England), Gabriel Zakuani (Northampton Town, England), Issama Mpeko (Kabuscorp, Angola), Joyce Lomalisa (Vita Club), Vital N’Simba (Bourg-Péronnas, Ufaransa), Fabrice N’Sakala (Alanyaspor, Uturuki), Chris Luyindama and Merveille Bope (TP Mazembe), Jordan Ikoko (Guingamp, Ufaaransa) na Marcel Tisserand (Ingolstadt, Ujerumani).
  Viungo: Youssouf Mulumbu (Norwich, England), Neeskens Kebano (Fulham, England), Rémy Mulumba (Ajaccio, Ufaransa), Hervé Kage (Kortrijk, Ubelgiji), Jacques Maghoma (Birmingham City, England), Paul-José M’Poku (Panathinaikos, Ugiriki), Jonathan Bijimine (Cordoba, Hispania) na Wilson Kamavuaka (Panetolikos, Ugiriki).
  Washambuliaji: Cédric Bakambu (Villarreal, Hispania), Dieumerci Mbokani (Hull City, England), Benik Afobe (Bournemouth, England), Firmin Mubele Ndombe (Vita Club), Junior Kabananga (Astana, Kazakhstan), Jordan Botaka (Charlton Athletic, England), Meschack Elia and Jonathan Bolingi (TP Mazembe), Ricky Tulengi (DCMP) na Jeremy Bokila (Al-Kharitiyath, Qatar).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BENIK AFOBE AITWA DRC KIKOSI CHA AWALI AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top