• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 26, 2016

  GEORGE MICHAEL AFARIKI DUNIA AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 53

  NYOTA wa Pop, George Michael amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa ana umri wa miaka 53 nyumbani kwake mjini Oxfordshire.
  Msemaji wa mwanamuziki huyo amesema kwamba 'amefariki dunia kwa amani' katika jengo lake la kifahari mjini Goring majira ya Saa 7.42 usiku.
  Meneja wa zamani wa Michael, Michael Lippman amesema kwamba amefariki kitandani baada ya 'moyo kusimama' 
  Thames Valley alisema Polisi walipigiwa simu kwenda nyumbani kwa marehemu Goring-on-Thames, Oxfordshire, kabla ya Saa 8:00 usiku katika siku ya Krisimasi.
  Buriani George Michael.  KWA HABARI ZAIDI, PICHA NA VIDEO GONGA HAPA KUSOA ZAIDI 
  Pamoja na kuanza kusumbuliwa na ugonjwa wa Nimonia tangu mwaka 2011, lakini Michael pia alikuwa anatumia dawa za kulevya ambazo zilikwishamuathiri vibaya. Mwaka 2008 alikuwa anavuta cocaine katika choo cha umma. 
  George Michael alizaliwa East Finchley, London, Juni 25, mwaka 1963 kabla ya kupata elimu yake katika shule ya Kingsbury High School Kaskazini mwa London. Mama yake, Lesley Angold, alikuwa dansa wa Kiingereza.
  Wakati akiwa mdogo, familia yake ilihamia Hertfordshire, katika kijiji kiitwacho Radlett kaskazini mashariki mwa Watford.
  Ni huko ambako alikutana na rafiki yake, mpiga gita Andrew Ridgeley baada ya kujiunga na shule ya Bushey Meads School mjini Bushey.
  Huku urafiki wao ukikua, ilikuwa wazi kwamba wawili wanataka kuwa wanamuziki maarufu na Michael akaanza rasmi harakati zake kama mwanamuziki anauetaka kuinuka.
  Alikuwa akiimba nyimbo ikiwemo Queen's '39' na kisha kuwa kama DJ. Akawa anakwenda kutumbuiza kwenye maonyesho madogo mjini Watford, Stanmore na Bushey.
  Kisha akaanzisha bendi ya The Executive na Ridgeley na kaka yake Ridgeley, Paul, Andrew Leaver na David Mortimer.
  Michael kisha akaanzisha Wham! na Ridgeley mwaka 1981 na albamu yao ya kwanza, Fantastic ilishika namba moja Uingereza miaka miwilo baadaye.
  Albamu yao ya pili, Make It Big – iliyokuwa na nyimbo kama 'Wake Me Up Before You Go-GO' - ilishika namba moja Marekani.
  Aliimba wimbo wa 'Do They Know It's Christmas' – ambao umekuwa wimbo namba moja wa Krisimasi UIngerea na duniani.
  Kundi la Wham! lilisambaratika mwaka 1986 na mwaka uliofuata akaanza kutembea kama mwanamuziki wa kujitegemea akimuibua Aretha Franklin aliyekuwa akifanya naye kazi.
  Akatoa albamu zake binafsi saba kuanzia Faith mwaka 1987 hadi Symphonica mwaka 2014. Wanamuziki wengi nyota wa kabla yake, wakati wake na baada yake wameguswa na kifo chake na kuandika kwenye mitandao ya kijamii wakimtakia ma;pumziko mapema. Buriani George.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GEORGE MICHAEL AFARIKI DUNIA AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 53 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top