• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 28, 2016

  LWANDAMINA AMUANZISHA ‘DOGO WA JKU’ LEO YANGA NA NDANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA George Lwandamina amemuanzisha kinda Emmanuel Martin katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Martin aliyesajiliwa dirisha dogo mwezi huu kutoka JKU ya Zanzibar ameanzishwa katika wingi ya kushoto ambayo mara nyingi huchezeshwa Deus Kaseke, ambaye leo anaanzia benchi.
  Na bila shaka Lwandamina amemuanzisha mchezaji huyo leo baada ya kucheza vizuri alipotokea benchi katika mchezo uliopita Yanga ikilazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon.
  Emmanuel Martin akiruka kuwania mpira wa juu katika mchezo dhidi ya African Lyon Ijumaa iliyopita 
  Emmanuel Martin akipiga krosi mbele beki wa African Lyon Ijumaa iliyopita 
  Emmanuel Martin akitafuta maarifa ya kumpita beki wa African Lyon  

  Kikubwa ni kwamba leo washambuliaji wote wawili tegemeo wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe wanaanza.
  Emmanuel Martin anaanza leo
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin.
  Katika benchi watakuwapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Andrew Vincent ‘Dante’, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa, Geoffrey Mwashuiya na Deus Kaseke.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AMUANZISHA ‘DOGO WA JKU’ LEO YANGA NA NDANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top