• HABARI MPYA

    Friday, December 30, 2016

    MICHO AMJUMUISHA JUUKO KIKOSI CHA AFCON 2017

    BEKI wa Simba Juuko Murshid amepenya kwenye kikosi cha mwisho cha Uganda kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Januari 2017 nchini Gabon. 
    Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameteua kikosi cha mwisho cha wachezaji 26, watakaokwenda Tunisia kesho ambako The Cranes itawekaa kambi hadi Januari 5 pamoja na kucheza na mchezo wa kirafiki.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Micho amesema kwamba kati ya hao, wachezaji 23 wameteuliwa moja kwa moja kuichezea Uganda kwenye AFCON ya kwanza baada ya miaka 39 na wanne ni wa akiba iwapo katika orodha ya awali itatokea mmoja ataumia au kupata dharula yoyote kabla ya kuanza mashindano.
    Juuko Murshid amepenya kwenye kikosi cha mwisho cha Uganda kitakachoshiriki AFCON Januari 2017 nchini Gabon

    Kocha huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda, El Hilal ya Sudan, Orlando Pirates ya Afria Kusini, Yanga ya Tanzania na St George ya Ethiopia, amewataja wachezaji wanne wa akiba ni Watenga Isma, Mukiibi Ronald, Vitalis Tabu na Nsibambi Derrick.
    Na kikosi kamili kinachokwenda Tunisia kesho ni; Odongkara Robert, Ochan Benjamin, Jamal Salim Magola, Iguma Denislawyer, Wadada Nicholas, Ochaya Joseph, Batambuze Shafiq, Juuko Murushid, Isinde Isaac na Waswa Hassan. 
    Wengine ni Qanyi Timothy, Aucho Khalid, Azira Mike, Mawejje Tony, Kizito Geoffrey, Oloya Moses, Mutyaba Muzamil, Walusimbi Godfrey, Kizito Luwaga Wiliam, Lubega Edrisa, Shaaban Mohammed, Serunkuma Geoffrey, Miya Farouk, Sentamu Yunus, Massa Geoffrey na Onyango Denis.
    Uganda, ambayo mara ya mwisho ilishiriki AFCON  mwaka 1978 na kuingia Fainali ikafungwa na Ghana 2-0, imepangwa Kundi D pamoja na Ghana, Mali na Misri. 
    Kwa ujumla Uganda imecheza fainali tano za AFCON, zikiwemo za mwaka 1962 iliposhika nafasi ya nne, 1968, 1974 na 1976 ilipokomea hatua ya makundi mara zote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AMJUMUISHA JUUKO KIKOSI CHA AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top