• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 28, 2016

  ZAHOR PAZI AMSHUKURU RAIS MALINZI KUMPATIA ITC YAKE AKIPIGE MBEYA CITY

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KIUNGO mshambuliaji mpya  wa Mbeya City FC, Zahor Pazi amemshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kufanikisha  kupatikana kwa hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)  iliyokuwa imekwama Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC) kwa miaka  miwili.
  Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Zahor amesema kuwa anafuraha kubwa kuona amerudi rasmi kwenye ulimwengu wa soka baada ya kukaa nje  kwa miaka miwili, licha ya jitihada kubwa alizokuwa akizifanya.
  Zahor Pazi amemshukuru Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa kufanikisha kupatikana kwa ITC yake 

  "Namshukuru Mwenyezi Mungu, hakika natanguliza sifa kwake, nimekuwa nje ya soka la ushindani kwa miaka miwili sasa, mara kadhaa nimejaribu kufanya jitihada za kuhakikisha naokoa kipaji changu lakini sikufanikiwa, namshukuru rais wa TFF amefanikisha  ndoto zangu za kuendelea kucheza mpira, niseme wazi  kuna wakati nilikata tamaa kabisa, ingawa pia niliendelea kujipa moyo na kumuomba Mungu, nashukuru sasa niko huru na naweza kuitumikia timu yangu mpya, alisema.
  Akiendelea  zaidi Zahor alisema  anawashukuru viongozi wa Mbeya City  Fc kwa kumpa nafasi ya kuitumikia timu hii licha ya kutokuwa kwenye soka la ushindani kwa muda mrefu.
  Nawashuruku viongozi wa mbeya city, wameniamini na wamenipa nafasi  ya kujiunga na timu licha ya kutokucheza kwa muda mrefu, najua sitakuwa na miujiza ila nitajitahidi kutumia uwezo wangu wote niliojaaliwa na Mwenyezi muMungu na kwa kushirikiana na wenzangu naamini tutaifikisha mbali timu yetu, alisema Zahor na kuongeza kuwa anaimani kubwa City itaibuka na ushindi dhidi ya Mbao Fc  jumamosi kufuatia mazoezi mazuri yaliyofanyia leo.
  Aidha Zahor  ametoa  wito kwa wachezaji wenzake kuwa makini katika hatua zote zinazohusu  usajili na uhamisho pale wanapohitaji  kutoka timu moja kwenda nyingine.
  Kwa wachezaji wenzangu kikubwa tuwe makini, nafahamu kuwa mara nyingi huwa tuna kiu kubwa ya kucheza nje, kila mmoja ana ndoto hizo  ni vyema kuangalia na kufanya mambo kwa makini, yaliyonikuta mimi  sikuyapanga ila kuna njia ambazo zilitumika ndivyo sivyo mpaka ikafika hapo ilipofika  hivyo ni vyema kuwa na watu makini na madhubuti ambao wanaosiamamia mambo yetu, alimaliza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZAHOR PAZI AMSHUKURU RAIS MALINZI KUMPATIA ITC YAKE AKIPIGE MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top