• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 27, 2016

  HAJIB MAMBO SAFI MISRI, WAARABU WAKOLEA...SASA WATAKA KUONGEA BIASHARA NA SIMBA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba amefuzu majaribio katika klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya Misri.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo kutoka mjini Alexandria yalipo makao makuu ya timu hiyo, Hajib alisema kwamba leo ameambiwa amefuzu majaribio yake baada ya siku tano.
  "Nimepewa majibu kwamba nimefuzu, kwa hiyo kinachofuata ni hii klabu kuzungumza na Simba ili wakubaliane kwanza, ndipo nitajua mustakabali wangu,"amesema Hajib.  

  Hajib (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Haras El Hodoud mazoezini leo mjini Alexandria 

  Hajib aliondoka Alhamisi iliyopita nchini kwenda Misri kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Simba. 
  Mshambuliaji huyo ameonyesha kiu ya kweli ya kutaka kucheza nje ya Tanzania, kwani katikati ya mwaka huu alikwenda Afrika Kusini kwa majaribio pia, ambako pamoja na kuripotiwa kufuzu katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJIB MAMBO SAFI MISRI, WAARABU WAKOLEA...SASA WATAKA KUONGEA BIASHARA NA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top