UMRI wa miaka 22 tu kijana wa Kitanzania kumiliki gari ka zaidi ya Sh. Milioni 100 labda liwe la urithi. Ama muuza 'ngada', au mwizi. Lakini Range Rover hiyo Sports pichani ni mali ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu.
Ulimwengu maarufu kama Rambo kwa jina la utani, anachezea klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika klabu hiyo ambako yupo katika mwaka wa nne sasa, Uli anacheza pamoja na Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta ambaye alikuwa wa kwanza kununua Range mwaka jana.
Wawili hao pamoja na kufurahia maisha TPM, lakini ndoto zao ni kusogea zaidi ya hapo na kwa muda sasa wamekuwa wakipigania kwenda Ulaya kwenye maslahi zaidi.
Samatta aliyewahi kuchezea Simba alinunua Range nyekundu na Ulimwengu aliyekaribia kusajiliwa Yanga SC kabla ya kwenda Mazembe, amenunua Range ya kijivu. Hongereni vijana. Mungu awafungulie zaidi.

![]() |
| Range la kijani la Thomas Emmanuel Ulimwengu likiwa limetulia |
![]() |
| Mbwana Ally Samatta alianza kununua Range nyekundu |
Wawili hao pamoja na kufurahia maisha TPM, lakini ndoto zao ni kusogea zaidi ya hapo na kwa muda sasa wamekuwa wakipigania kwenda Ulaya kwenye maslahi zaidi.
Samatta aliyewahi kuchezea Simba alinunua Range nyekundu na Ulimwengu aliyekaribia kusajiliwa Yanga SC kabla ya kwenda Mazembe, amenunua Range ya kijivu. Hongereni vijana. Mungu awafungulie zaidi.
![]() |
| Wazee wa Range; Kutoka kulia Thomas Ulimwengu, Mahmoud Zubeiry na Mbwana Samatta |

.png)
0 comments:
Post a Comment