• HABARI MPYA

    Wednesday, July 01, 2015

    SIMBA SC WAZINDUA KADI MPYA LEO DAR

    KLABU ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua kadi mpya za wanachama ambazo zinamwezesha kila mwanachama wa Simba kupata bima ya maisha hadi Tsh 250,000 ikiwa atafiwa na mwenza au mtoto au yeye mwenyewe kupitia bima ya maisha iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba leo hii imezindua Kadi za watoto yaani Simba Cubs.
    Akizungumza wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendaji ikifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita hapa kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaotaka kuwa wanachama wa Simba’’.
    Aliongeza kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuapply kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz/fomu . Napenda mtambue hii ni historia katika ukanda huu kuweza kutumia teknojia kufikia wanachama, Sisi ni wakisasa na tunaona mbele!.
    Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya masoko na biashara Imani Kajula alisema
    "Uanzishwaji wa Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto sio tu kutambuliwa kuwa memba wa Simba, bali pia kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio yanayoandaliwa na Simba Sports Club. Pia maduka mbalimbali yatatoa punguzo kwa watoto wenye Simba Cub Card.
    Wote mnajua fika kuwa mapenzi hujengwa, Simba inalenga kujenga msingi imara wa kuendeleza wanachama na wapenzi wake’’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAZINDUA KADI MPYA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top