• HABARI MPYA

    Wednesday, July 01, 2015

    MAZEMBE YAKIRI KUPOKEA OFA YA KUMUUZA UFARANSA KALABA, LAKINI KATUMBI ALETA ‘MIZENGWE’ KIBAO

    KLABU ya TP Mazembe imethibitisha kupokea ofa ya klabu ya Lille ya Ufaransa kumtaka Nahodha wa Zambia, Rainford Kalaba (pichani kulia).
    Mwenyekiti wa Mazembe, Moise Katumbi amesema kwamba mabingwa hao wa Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC) wanaitathmini ofa ya Lille kwa Kalaba.
    Kalaba amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Lille, kufuatia kocha wa zamani wa Zambia, Herve Renard kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Ligi Kuu nchini humo, maarufu kama Ligue One Mei mwaka huu.
    “Lille inamtaka Kalaba aende huko na tupo kwenye mazungumzo juu ya safari ya Lille,” amesema Katumbi.
    “Sasa tatizo ni tunataka mustakabali mzuri kwa Kalaba. Tunatazama hilo kama Kalaba atakwenda huko ili mradi tu au kwa mustakabali mzuri.
    “Unatakiwa kuangalia mustakabali na ada ya uhamsho kwa Kalaba, kwa sababu unajua mchezaji anapotoka Afrika wanatoa fedha kidogo na hiyo ndiyo inayoziua timu nyingi (kwa Afrika).”
    Kalaba amekuwa mchezaji wa Mazembe tangu mwaka 2010 alipojiunga na timu hiyo ya Lubumbashi yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa mkopo kutoka Sporting Braga ya Ureno, kabla ya kusaini Mkataba wa moja kwa moja mwishoni mwa msimu wake wa kwanza DRC.
    Kiungo huyo wa Zambia alikuwa mfungaji bora wa Mazembe msimu wa 2013/2014 kwa mabao yake tisa, akiisaidia timu ya Lubumbashi kubeba taji la nne mfululizo na la 14 la Ligi ya DRC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZEMBE YAKIRI KUPOKEA OFA YA KUMUUZA UFARANSA KALABA, LAKINI KATUMBI ALETA ‘MIZENGWE’ KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top