• HABARI MPYA

    Tuesday, June 09, 2015

    YAYA TOURE ATEMWA IVORY COAST UFUNGUZI KUFUZU AFCON

    KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure ametemwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kitakachomenyana na Gambia katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwishoni mwa wiki kwa sababu ya majeruhi.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Ivory Coast imesema jana kwamba Nahodha huyo wa Tembo hatakuwamo kwenye kikosi hicho kwa sababu ya majeruhi.
    Toure alionekana kumaliza msimu wa Ligi Kuu ya England akiwa na klabu yake, Manchester City mwezi uliopita bila tatizo lolote.
    Pamoja na hayo, shirikisho la soka la nchi hiyo limesema ni majeruhi bila kutoa taarifa zaidi.
    Midfielder Yaya Toure has been left out of Ivory Coast's squad for this weekend's African Nations Cup qualifier
    Kiungo Yaya Toure ameenguliwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kitachomenyana na Gambia mwishoni mwa wiki kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika

    Kocha wa muda wa Tembo, Ibrahima Kamara pia atamkosa kaka yake Yaya, Kolo Toure, ambaye amestaafu soka ya kimataifa baada ya kuiwezesha Ivory Coast kutwaa Kombe la AFCON nchini Equatorial Guinea mwanzoni mwa mwaka huu.
    Kikosi cha Tembo kitasafiri hadi Libreville kikiwa na nyota wengine akiwemo mchezaji mwenzake Yaya pale Man City, Wilfried Bony, Gervinho na Salomon Kalou, ambao walikuwemo kwenye timu iliyobeba Kombe la Mataifa ya Afrika Februari.
    Mchezo wa Jumapili mjini Libreville ni sehemu ya mechi za ufunguzi za mbio za AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.
    Salmon Kalou has been named in the Ivory Coast squad
    Manchester City striker Wilfried Bony has been named in the Ivory Coast squad
    Roma winger Gervinho has been called up to Interim coach Ibrahima Kamara's side

    Salomon Kalou, Wilfried Bony na Gervinho wote watakuwemo kwenye kikosi cha Ivory Coast
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE ATEMWA IVORY COAST UFUNGUZI KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top