• HABARI MPYA

    Tuesday, June 09, 2015

    DANI ALVES AONGEZA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI BARCELONA

    BEKI Dani Alves (pichani kushoto) leo amemaliza utata juu ya mustakabali wake, baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuchezea mabingwa wa Ulaya, Barcelona.
    Mkongwe huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 32, Mkataba wake wa sasa ulitarajiwa kumalizika Juni 30, lakini amefikia makubaliano na na uongozi wa Barca kuongeza hadi mwaka 2017, huku kukiwa na nafasi ya kurefushwa kwa mwaka mmoja zaidi.
    Alves, ambaye alijiunga na timu hiyo ya Katalunya kutoka Sevilla mwaka 2008, hadi sasa ameichezea Barca mechi 343, idadi ambayo ni kubwa kuliko mchezaji mwingine yeyote wa kigeni katika historia ya klabu hiyo.
    Katika kipindi hicho ameshinda mataji 19, yakiwemo matano ya La Ligas, matatu ya Ligi ya Mabingwa, matatu ya Vikombe vya Hispania, mawili ya Super Cup ya Ulaya, manne ya Super Cup ya Hispania na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia.
    Ni sehemu ya wachezaji saba waliokuwamo kwenye vikosi vilivyoshinda mataji matatu kwa mpigo msimu mmoja: cha sasa kikiwa cha msimu huu kilichokamilisha taji la tatu kwa kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki mjini Berlin kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Juventus.
    Awali msimu wa 2008-2009, alikosa fainali ya Kombe la Ulaya mjini Rome dhidi ya Manchester United kutokana na kuwa akitumikia adhabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DANI ALVES AONGEZA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top