KIUNGO Xavier ‘Xavi’ Hernandez Creus Jumamosi ya Juni 6 alicheza mechi yake ya mwisho Barcelona akitokea benchi dakika ya 78 kwenda kuchukua nafasi ya Andres Iniesta katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015.
Xavi aliisaidia Barca kutwaa taji lake la tano la michuano hiyo wakiifunga Juventus ya Italia mabao 3-1 Uwanja wa Olympiki mjini Berlin, Ujerumani.
Hiyo iliifanya Barcelona kuwa klabu ya kwanza kihistoria kushinda mara mbili mataji yote, mawili ya mashindano ya nyumbani na moja la Ulaya, huku Xavi, Iniesta, Lionel Messi, Gerard Pique, Pedro Rodriguez, Sergio Busquets na Dani Alves wakiwa wachezaji pekee waliokuwamo kwenye vikosi vyote vilivyofanya hivyo.
Baada ya mafanikio hayo, Xavi aliyezaliwa Januari 25 mwaka 1980 anahamia Al Sadd ya Qatar kwenda kumalizia soka yake.
Mzaliwa huyo wa mji wa Terrassa, Barcelona, Katalunya, ni zao la akademi ya Barcelona, iitwayo La Masia ambayo alijiunga nayo akiwa ana umri wa miaka 11.
Huyu ni mchezaji ambaye aliibuliwa na Barcelona na alipewa heshima zote wakati anajiandaa kuondoka karibu mwezi mzima sherehe za kumuaga zilifuatana.
Jumamosi usiku wakati natazama fainali ya Ligi ya Mabingwa, hususan Xavi wakati anaingia kumpokea Iniesta na nilipokumbuka historia yake, nilijihisi nami ni sehemu ya wana Barcelona.
Hata kama wewe ni shabiki wa timu nyingine, lakini unawezaje kuepuka kuipenda Barcelona kwa mambo mengi tu, kubwa sera na falsafa zake zilizoenziwa.
La Masia inaweza kuwa akademi maarufu zaidi ya soka duniani, iliyoibua mchezaji kutoka sayari nyingine, Lionel Messi.
Messi alizaliwa Juni 24, mwaka 1987 mjini Rosario, Santa Fe Province, Argentina, alianza kucheza soka akiwa ana umri wa miaka mitano katika timu ya Grandoli ya nyumbani kwao, iliyokuwa ikifundishwa na baba yake, Jorge.
Mwaka 1995, Messi akahamia Old Boys ya Newell, nyumbani kwao kabisa, Rosario na akiwa na umri wa miaka 11, River Plate ilimtamani, lakini haikuwa tayari kumlipa dola za Kimarekani 900 kwa mwezi.
Mkurugenzi mmoja wa Barcelona, Carles Rexach akaanza kufuatilia kipaji cha Messi na huo ukawa mwanzo wake wa kujiunga na akademi ya Barcelona na sasa ni gwiji wa klabu.
Lakini bado Barcelona imeendelea kununua kwa bei kubwa tu wachezaji nyota wa timu nyingine- mfano Ivan Rakitic, Luis Suarez na Neymar wafungaji mabao ya fainali dhidi ya Juve.
Unaweza ukawa shabiki mzuri wa timu nyingine, hata wapinzani wao, Real Madrid- lakini bado ukavutiwa na Barcelona kwa sababu kibao.
Soka yao tamu ya pasi nyingi za kuburudisha, hiyo pekee imeifanya kila timu duniani itamani kuwa kama Barca.
Barca imewaharibu hadi mashabiki wa Tanzania, sasa wanapenda pasi nyingi. Na viongozi wa klabu kubwa nchini, Azam FC, Simba na Yanga wamekuwa wakitamani soka ya Barca kiasi kwamba wanatafuta aina ya makocha wa kufundisha mpira wa aina hiyo.
Makocha wanafukuzwa kila kukicha Azam FC, Simba na Yanga SC kwa sababu nyingi, kubwa hawafundishi soka ya kuvutia kama ya Barca.
Lakini kitu kimoja tu kwa Barca klabu zetu zimeshindwa kuiga- uwekezaji katika soka ya vijana kuanzia wakiwa wadogo kama Xavi au Messi.
Azam FC wana akademi nzuri pale Chamazi, lakini bado hawajawa na mfumo na sera bora kama zile za La Masia.
Simba na Yanga wao ndiyo kabisa- hawana mpango na akademi. Hivyo viwanja tu japo vya kufanyia mazoezi ya timu zao za wakubwa hawana.
Hivi karibuni ulitokea mzozo baina ya mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ na Simba SC, klabu ikidai ilimuibua mchezaji huyo aliyekuwa analalamikia ‘kubambikiwa’ Mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.
Messi alitoka Bom Bom kujiunga na Simba SC akiwa tayari mchezaji kijana wa miaka isiyopungua 17- Simba wanawezaje kusema walimuibua?
Waseme wameendeleza kipaji chake- hapo sawa. Leo Simba waseme wamemuibua Messi na Barcelona watasemaje kwa ‘Messi Orijino’?

.png)
0 comments:
Post a Comment