• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2015

    NIGERIA YAPAA KILELENI KUNDI LA TAIFA STARS KUFUZU AFCON

    NIGERIA imeanzia kileleni mwa Kundi G baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chad mechi ya ufunguzi kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 jana uwanja wa Ahmadu Bello,
    Kaduna.
    Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Gbolahan Salami dakika ya 63 na O Ighalo kwa penalti dakika ya 80.  
    Mechi nyingine ya Kundi G inazikutanisha wenyeji Misri dhidi ya Tanzania leo mjini Alexandria. 
    Katika mechi nyingine za jana, Algeria iliifumua mabao 4-0 Shelisheli, Mali imeifunga 2-0 Sudan Kusini, Senegal imeifunga 3-1 Burundi na Burkina Faso imeichapa 2-0 Comoro.
    Afrika Kusini imelazimishwa sare ya 0-0 na Gambia, Cape Verde imeichapa 7-1 Sao Tome, Angola imeipiga 4-0 Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda, imeifunga Botswana mabao 2-0, Zambia imelazimishwa sare ya 0-0 Guinea-Bissau na Malawi imefungwa 2-1 na Zimbabwe.
    Mechi za juzi Tunisia iliifunga mabao 8-1 Djibouti, Morocco ilishinda bao 1-0 dhidi ya Libya na Swaziland walishinda 2-1 dhidi ya Guinea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA YAPAA KILELENI KUNDI LA TAIFA STARS KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top