TIMU ya taifa ya Argentina imelazimishwa sare ya 2-2 na Paraguay katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataia ya Amerika Kusini, Copa America 2015 michuano inayoendelea nchini Chile tangu Juni 11, mwaka huu.
Sergio Aguero alianza kuifungia Argentina dakika ya 29, kabla ya Lionel Messi kufunga la pili kwa penalti dakika ya 36, kufuatia Angel di Maria kuchezewa rafu na Miguel Samudio.
Paraguay ikafanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Nelson Valdez dakika ya 60 na Lucas Barrios dakika ya 90. Katika mchezo uliotangulia wa kundi hilo jana, Uruguay ilishinda 1-0 dhidi ya Jamaica bao pekee la James Rodriguez dakika ya 51.
Mechi za ufunguzi za mashindano hayo, juzi za Kundi A, wenyeji Chile waliwafunga 2-0 Ecuador na Mexico walilazimishwa sare ya 0–0 na Bolivia.
Mechi za kwanza za Kundi C, zinafanyika leo Colombia na Venezuela na Brazil na Peru.
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Roncaglia, Garay, Otamendi, Rojo, Banega/Biglia dk80, Mascherano, Pastore/Tevez dk76, Messi, Aguero/Higuain dk76 na Di Maria.
Paraguay: Villar, M Caceres, Da Silva, Aguilar, Samudio, Bobadilla/Benitez dk66, V Caceres, Ortigoza, Ortiz/Gonzalez dk46, N Valdez, Santa Cruz/Barrios dk79.
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Argentina kwa penalti jkatika sare ya 2-2 na Paraguay PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment