![]() |
| Joseph Mahundi akikaabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Desemba mwaka jana na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia |
Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Hii inakuwa mara ya pili kwa Mahundi kuibuka mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu, kwani Desemba mwaka jana pia alishinda tuzo hiyo.
Ligi Kuu ilimalizika Mei mwaka huu, Yanga SC wakitwaa ubingwa, Azam FC nafasi ya pili na Simba SC nafasi ya tatu, Mbeya City ya nne wakati Coastal Union ilimaliza nafasi ya tano.



.png)
0 comments:
Post a Comment