Na Mahmoud Zubeiry, MWANZA
ILALA imetwaa ubingwa wa mashindano ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 13 baada ya kuifunga mabao 3-2 Alliance Academy ya Mwanza katika mchezo wa fainali jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.
Mashindano hayo maalum yaliyodumu kwa wiki moja, yaliandaliwa ili kuunda timu ya taifa itakayoandaliwa kwa ajili ya Fainali za Afrika mwaka 2019 ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji na hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Alliance walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tisa mfungaji Alphonce Mabula kabla ya Ilala kusawazisha dakika ya 20, mfungaji Morris Michael Njaku ‘Chuji’.
Katika mchezo huo uliochezwa kwa dakika 30 kila kipindi- Ilala walirudi vizuri zaidi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 40 mfungaji Chuji tena.
Feisal Awadh Salum ‘Coutinho’ aliifungia Ilala bao la tatu dakika ya 50 kabla ya Alliance kupata bao la pili dakika za majeruhi.
Alliance waliuanza mchezo vizuri dakika 10 za mwanzo, wakionekana kuwazidi nguvu Ilala, ambao baadaye walibadilisha mbinu na kutumia washambuliaji wawili badala ya mmoja, hatimaye kuuteka mchezo.
Mgeni rasmi katika mchezo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi aliwapongeza Ilala kwa kuwa mabingwa na pia Alliance kwa kushika nafasi ya pili.
Malinzi akasema anaamini vijana hao watakuwa kuibeba soka ya Tanzania kuanzia miaka mine ijayo.
Katika mchezo uliotangulia, Kinondoni walifanikiwa kupata nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mara kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya 0-0.

![]() |
| Fesal Salum (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Ilala bao la tatu. Kushoto ni mfungakji wa mabao mawili ya timu hiyo, Morris Njaku akimfuata mwenzake kushangilia naye |
![]() |
| Wachezaji wa Ilala wakishangilia baada ya mechi |
![]() |
| Morris Njaku akimtoka beki wa Alliance Academy |
![]() |
| Feisal Salum akitafuta maarifa ya kumtoka Gasper Gombanila wa Alliance Academy |
Katika mchezo huo uliochezwa kwa dakika 30 kila kipindi- Ilala walirudi vizuri zaidi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 40 mfungaji Chuji tena.
Feisal Awadh Salum ‘Coutinho’ aliifungia Ilala bao la tatu dakika ya 50 kabla ya Alliance kupata bao la pili dakika za majeruhi.
Alliance waliuanza mchezo vizuri dakika 10 za mwanzo, wakionekana kuwazidi nguvu Ilala, ambao baadaye walibadilisha mbinu na kutumia washambuliaji wawili badala ya mmoja, hatimaye kuuteka mchezo.
Mgeni rasmi katika mchezo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi aliwapongeza Ilala kwa kuwa mabingwa na pia Alliance kwa kushika nafasi ya pili.
Malinzi akasema anaamini vijana hao watakuwa kuibeba soka ya Tanzania kuanzia miaka mine ijayo.
Katika mchezo uliotangulia, Kinondoni walifanikiwa kupata nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mara kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya 0-0.

.png)
0 comments:
Post a Comment