• HABARI MPYA

    Saturday, June 13, 2015

    UGANDA YAANZA VYEMA KUFUZU AFCON 2017, YAICHAPA BOTSWANA 2-0

    TIMU ya taifa ya Uganda, imeanza vyema mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017, baada ya kuifunga Botswana mabao 2-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi D Uwanja wa Taifa wa Mandela mjini Kampala jioni ya leo.
    Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo Geoffrey Massa na Brian Umony (pichani) yote kipindi cha pili.
    Uganda waliingia katika mchezo huo wakipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi yao nzuri hivi karibuni nyumbani wakiwa wameshinda mechi zote saba.
    Nahodha wa kikosi cha kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’, Massa alifunga bao la kwanza dakika ya 54, akimalizia krosi ya Luwagga.
    Dakika 10 baadaye mshambuliaji wa zamani wa Azam FC ya Tanzania, Umony akaifungia bao la pili The Cranes dakika ya 64.
    Katika mechi nyingine ambazo zimekwishamalizika, Zambia imelazimishwa sare ya 0-0 Guinea-Bissau Uwanja wa Levy Mwanawasa na Malawi imefungwa 2-1 na Zimbabwe nyumbani, Uwanja wa Kaamuzu. Bao la Malawi lilifungwa na John Banda dakika ya 25 baada ya Cuthbert Malajila kuanza kuifungia Zimbabwe dakika ya 24. Shujaa wa mchezo alikuwa Khama Billiat aliyeifungia Zimbabwe bao la ushindi dakika ya 83.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YAANZA VYEMA KUFUZU AFCON 2017, YAICHAPA BOTSWANA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top