• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  NYOTA WAZIDI KUIKIMBIA GOR MAHIA, KIZITO NAYE AMFUATA SSERUNKUMA KUHAMA KENYA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  KLABU ya Gor Mahia inakabiliwa na hatari ya kupoteza nyota wake zaidi, kutokana na kiungo Mganda Geoffrey Baba Kizito kuweka wazi anawaacha mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya 2014 na kwenda Vietnam.
  Kizito aliyejiunga na Gor Mahia mwanzoni mwa msimu wa 2014, mara moja alikuwa tegemeo la klabu hiyo kiasi cha kuisaidia kutetea ubingwa wa KPL.
  Yeye mwenyewe binafsi, pia akafanikiwa kushika nafasi ya pili katika tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka Kenya na Kiungo Bora wa KPL.
  Geoffrey Baba Kizito anaondoka Gor Mahia

  Akizungumza na BIN ZUBEIRY mwishoni mwa wiki, kiungo huyo hodari amesema kwamba ataondoka K’Ogalo kwenda klabu ya Vietnam, ambayo hata hivyo hakuitaja jina
  “Nafikiri nimetoa mchango wangu kuisaidia timu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya na ninaangalia mipango mingine kwa sasa. Nimesaini Mkataba wa awali na timu Vietnam na ni matumaini yangu nitarudi huko,”amesema Kizito ambaye amewahi kuchezea Saigon Xuan ya Ligi Kuu ya Vietnam.
  Iwapo Kizito ataondoka, litakuwa pigo kubwa kwa Gor, kwani tayari tegemeo lake mabao, Mganda Dan Sserunkuma anaelekea kukamilisha mipango ya kujiunga na Simba SC ya Tanzania.
  Sserunkuma alikuwa Tanzania wiki iliyopita kwa mazungumzo kabla ya kurejea Uganda na kesho anatarajiwa kutua tena Dar es Salaam kusaini Mkataba wa mwaka mmoja na moja kwa moja kuanza kazi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA WAZIDI KUIKIMBIA GOR MAHIA, KIZITO NAYE AMFUATA SSERUNKUMA KUHAMA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top