• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.
  Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.
  Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba 20 mwaka huu.

  Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20 na wasiopungua 16.
  Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.
  Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top