• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  BALOTELLI AOMBA RADHI KWA KAULI TATA INSTAGRAM

  MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario Balotelli, ameomba radhi kwa kuweka picha yenye kuashiria vitendo vya kibaguzi katika ukurasa wake wa Instagram. 
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 24, mwenye matukio mengi ya utukutu, haraka alifuta picha hiyo iliyokuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.
  “Ninaomba radhi kwa yoyote aliekwazika. Nilifikiri kuwa ilikua ni ucheshi na sio ubaguzi ,sikujua kama inaweza kuwa na athari”.
  Nyota huyo wa zamani wa Manchester City na AC Milan atakosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Leicester City sababu ni majeruhi na ametakiwa na FA kutoa utetezi wake hadi kufika Ijumaa, vinginevyo anaweza kufungiwa mechi tano.
  Balotelli has not impressed at Liverpool since arriving this summer and is yet to score a Premier League goal
  Balotelli ameomba radhi kwa kile alichoposti kwenye ukurasa wake wa Instgram

  Katika taarifa yake aliyoposti kwenye akaunti yake ya Twitter, mchezaji saying: "Ninaaomba radhi kama nimemkwaza yeyote. Posti hiyo ilikuwa na maana ya kupinga ubaguzi na kuchekesha. Sasa naelewa kwamba nje mazngira halisi kunaweza kuwa na madhara mengine. Siyo kila Mmexico ana mustachi, siyo kila mtu mweusi anaruka juu na siyo kila Myahudi anapenda fedha. 
  "Nilitumia katuni iliyotongenezwa na mtu mwingine kwa sababu ilikuwa ina Super Mario na nafikiri ilikuwa fani na si ya kukera. Tena, samahani," amesema. 
  Balotelli wrote this apology on Twitter on Tuesday morning, claiming his post was meant to be 'anti-racist'
  Huu ndiyo ujumbe ambao Balotelli ameweka kwenye akaunti yake ya Twitter
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOTELLI AOMBA RADHI KWA KAULI TATA INSTAGRAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top