KIUNGO wa Barcelona, Xavi anaamini mchezaji mwenzake nyota, Lionel Messi anaweza kuwa 'babu kubwa' hata kwenye Ligi Kuu ya England kuliko alivyo sasa kwenye La Liga.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye ameshinda mataji saba ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wake katika klabu hiyo, anaamini falsafa ya ulinzi ya England itampa fursa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutamba.
Ameiambia BBC Michezo: "Nafikiri atakuwa mzuri hata kwenye Ligi Kuu (England) kwa sababu haina ulinzi mkali,".
Lionel Messi amejipambanua kama mchezaji wa kipekee duniani akiwa Barcelona
"Wakati wanapojilinda dhidi ya Barcelona, wao [Klabu za England] wanacheza mfumo wa mmoja dhidi ya mmoja, wanakaba kwa kujituma na kutumia nguvu nyingi. Lakini Leo anaweza kupata nafasi nyingi kuliko La Liga,".
Licha ya maelezo hayo ya Xavi, inaonekana kama Messi hana mango kabisa wa kuhamia Ligi Kuu ya England, katakana na kurudia kusema anafurahia kubaki Barcelona kumalizia soka yake huko.
Messi alifunga bao lake la kwanza kwenye ardhi ya England Uwanja wa Wembley mwaka 2011 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Man United
Xavi ana Messi wakijadiliana kabla ya kupiga mpira wa adhabu katika mechi ya La Liga dhidi ya Rayo Vallecano
Kwa msimu huu, mshambuliaji huyo wa Argentina tayari amefunga mabao 11 katika mechi 15 za vigogo hao wa Katalunya, wakiwa wanazidiwa pointi mbili na wapinzani wao, Real Madrid waliopo kileleni mwa La Liga.
Messi pia anakaribia kuvunja rekodi nyingine baadaye mwezi huu, kwa kumpiku Raul kwa ufungaji wa mabao mengi zaidi katika katika Ligi ya Mabingwa (mabao 71), baada ya kufinikiwa kumfikia kutokana na kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ajax mapema mwezi huu.


.png)
0 comments:
Post a Comment